Kutokana na kuwepo na kilio cha Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini kudai kuibiwa fedha wanazozipata kutoka kwenye mradi huo na ndugu zao wa karibu, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Dunstan Kyobya ameielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara—Mikindani kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaojihusisha na wizi huo huku akimtaka kuainisha kaya zenye wazee sana ambazo haziwezi kutunza fedha na kuhakikisha fedha zao hazipotei.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo OKtoba 19,2022 alipozungumza na walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya masikini waliopo Kata ya Chikongola na Tandika.
Aidha Mhe.Mkuu wa Wilaya amewataka walengwa wote kuendelea kushiriki kwenye miradi ya ajira ya muda inayolenga kuwapatia kipato kupitia nguvu kazi katika miradi inayoibuliwa lakini pia kushiriki katika shughuli mbalimbalim za Maendeleo ili Mnauspaa weze kukua.
Ameendelea kuwasisitiza wataalamu wa Manispaa aya Mtwara-mikindani kuhakikisha wanaisimamia miradi ya TASAF vizuri na kuwataka kuendelea kutoa elimu juu ya mradi huo ili faida yake iwafikie walengwa wote.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amempongeza Mratibu wa TASAF Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani Bi.Sylivia Mwananche kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuhakikisha mradi huo unakwenda vizuri huku akisisitiza elimu zaidi ya Mpango wa kunusru Kaya masikini itolewe kwenye kila vikao vya mtaa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Tandika Mhe.Haruni Haruni ameishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha za kuhudumia wazee na kutoa rai kwa walengwa wa Mpango huo kuhakikisha wanaitunza na kuilinda miradi yote inayotekelezwa na mpango huo ili iweze kuleta Manufaa kwa wote.
Nae Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Sylivia Mwanache amesema kuwa Serikali imekuwa ikileta fedha za walengwa wa Mpango kwa wakati na amewaomba walengwa kuwa watulivu pale fedha inapotokea mara chache fedha ikachelewa.
Akizungumza kwa naiba ya walengwa wengine Bi. Clara Kmatwanje ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapatia fedha za TASAF ambazo zinawasaidia katika kujikimu kimaisha Pamoja na kuwasomesha Watoto wao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.