Kutokana na tabia ya baadhi ya watu kwa makusudi wanaiba na kuharibu nguzo zilizosimikwa kwenye zoezi la operesheni ya anuani za makazi kwenye maeneo yetu, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mtwara (OCD) kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kufanya uharibifu huo.
Ili watu hao waweze kubainika Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa Kata,Mitaa, Kituo cha Polisi na ofisi ya Mkurugenzi ili waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Wilaya ametoa onyo hilo April 30,2022 kwneye mkutano wa baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani lililoketi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Call and Vision.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi wa Manispaa kila mmoja katika eneo lake kuhakikisha anaisemea vizuri Mtwara kwa kusema mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan.
“Sisi wenyewe ni mashahidi, Serikali imeleta miradi mingi ya maendeleo ndani ya Manispaa yetu, vipo vituo vya afya, madarasa, nyumba za walimu Pamoja na miradi mingine mingi, twendeni tukawaambie wananchi mazuri yanayofanywa na serikali yetu”.
Kuelekea kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika Agosti 23 mwaka huu Mhe. Mkuu wa Wilaya pia amewaomba Madiwani kuandaa mikutano kwenye maeneo yao na kufanya uhamasishaji juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.