Kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, , Leo Machi 7 wanawake wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutoka kwenye Taasisi mbalimbali wamekabdihi shuka 122 za hospitali na vifaa 5 vya kupimia mapigo ya mtoto awapo tumboni (Fetoscope) kwa Mstahiki Meya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile ambae pia amevikabidhi vifaa hivyo kwa mganga Mkuu wa Manispaa Dkt. Joseph Kisala ili aweze kuvigawa kwenye vituoa vya afya na zahanati zilizopo.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mstahiki Meya amewashukuru wanawake wote kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa kutoa vifaa vya hospitali kwani vitasaidia kupunguza changamoto zilizopo.
Taasisi zilizokabidhi mashuka ni pamoja na TANESSCO mashuka (20), Bandari (32), Mati Naliendele(10), MSD (15), pamoja na bodi ya koroshoTanzania wamekabidhi mashuka 45.
Maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu kimkoa yanafanyika Manispaa ya Mtwara-Mikindani yakiwa na kauli mbiu inayosema "Kizazi Cha haki na usawa kwa Maendeleo endelevu, Tujitokeze Kuhesabiwa"
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.