Kueleka kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, wanawake wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Leo Machi 7,2021 kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali wamekabidhi nyumba ya makazi kwa bibi na babu Chikaoneka (walemavu wa viungo) wanaoishi Mtaa wa Mjimwema , katika Kata ya Magengeni.
Nyumba hiyo ambayo imegharimu shilingi 9,481,000 imejengwa kwa nguvu za wanawake hao Pamoja na taasisi zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani baada ya kuona wazee hao kuwa na uhitaji wa makazi bora na y a kisasa kuliko makazi walikuwa wanaishi awali.
Mkuu wa Wailaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ametoa pongezi kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Juliana Manyama kwa kuweza kuwaunganisha wanawake hao na kujenga nyumba iliyokabidhiwa kwa wazee hao.
Katika kuhakikisha kuwa wazee wanapata huduma zote za Msingi ikiwemo maji, umeme na barabara Mkuu wa Wilaya ameziagiza Taasisi husika za TARURA, TANESCO, MTUWASA na TFS kuhakikisha hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu huduma hizo ziwe zimeshapelekwa na zitagharamiwa na Ofisi yake.
Babu na Bibi Chikaoneka ni mume na mke ambao wote ni walemavu wa viungo na katika Maisha yao hawakujaliwa kupata Watoto hivyo wanaishi peke yao bila ya kupata msaada kutoka ndugu
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.