Kupitia mradi wa upimaji na upangaji wa ardhi unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la kusaidia wanawake (UN WOMEN), Wataalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya jamii, ardhi na sheria Manispaa ya Mtwara-Mikindani wakitoa elimu itakayomuwezesha mwanamke kutambua haki yake katika umiliki wa ardhi kihalali kwa wanawake wa Mtaa wa Naulongo na Pwani B iliyopo Kata ya Naliendele.
Shirika la UN WOMEN limeleta mradi huo ili kumuwezesha mwanamke kiuchumi ikiwemo kumsaidia kutambua ardhi yake na kuirasimisha ardhi hiyo bila gharama yoyote ili awe na nyaraka halali za umiliki ambazo zitamsadia hapo baadae.
Pamoja na Mitaa ya Naulongo na Pwani B Mitaa mingine ambayo inapitiwa na mradi huo ni pamoja na Mtaa wa Ligula B na Majengo iliyopo Kata ya Chuno pamoja na Mtaa wa Mahuta na Lwelu iliyopo Kata ya Jangwani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.