Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya, amewataka wanawake mkoani Mtwara kusimamia vyema maadili ya Watoto na vijana ili kuliepusha Taifa na kasi ya mmomonyoko wa maadili unaoendelea kuikumba Dunia.
Mwaipaya amesema hayo wakati wa hotuba yake aliyoitoa mapema leo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mashujaa, Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Alisema kwasasa linakumbwa na wimbi la mapokea ya kimaadili yanayochagizwa na ukuaji wa maendeleo ya kiteknolojia, ikiwemo masuala ya ndoa za jinsia moja, hivyo wanawake watumie nguvu yao ushawishi katika malezi kukemea vitendo hivyo na kuifanya dunia kuendelea kuwa sehemu salama kuishi.
Aidha, aliwasisitiza wanawake hao kuendelea kutoa ushirikiano katika shughuli zote za maendeleo kielimu kwenye maeneo yao ili kuweza kupata maendeleo yanayotarajiwa na kwa wakati.
Vilevile alitumia jukwaa hilo kuwapongeza wanawake kote nchini kwani mpaka sasa takwimu zinaonyesha wanawake ndio vinara katika sekta ya uzalishaji nchini.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.