Kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani yanayofanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, Manispaa ya Mtwara-Mikindani imesherehekea siku hii kipekee kwa kuwashika mkono wanawake wenye mahitaji maalumu kwa kuwapatia vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 7.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Machi 7, 2021 katika viwanja vya Mashujaa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi. Juliana Manyama amesema kuwa vifaa vilivyotolewa vimelenga kuwarahisishia wanawake hao utendaji wa wa shughuli zao za kila siku za kujitafutia kipato.
Manyama amevitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni pamoja na baisklei tatu za watu wenye ulemavu, kadi za bima ya afya ya jamii iliyoboteshwa kwa watu 312 ambayo ni sawa na kaya 52 zenye mazingira magumu.
Vifaa vingine ni Pamoja na magodoro kumi na sita na chakula kwa kaya zinazoongozwa na wanawake zilizopata athari kwenye mvua zilizonyesha Januari mwaka huu Pamoja na mchango wa matofali mia tano na bati ishirini na tano zilizotolewa kwa mwanamke mlemavu ambae makazi yake yamebomolewa na mvua hizo.
Vifaa vyote hivi vimetolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo taasisi za kiserikali na watu binafsi Pamoja na wananchi kutoka katika Kata na Mitaa iliyopo Manispaa.
Wakizungumza mara baada ya kupokea vifaa hvyo Bi. Liza Kibwana amewashukuru wanawake wa Mtwara-Mikindani kwa kumuwezesha baiskeli ambayo itamsaidia kwenye shughuli zake za ujasiriamali.
Nae Scholastika Polycarp mwananfunzi mwenye ulemavu kutoka shule ya Msingi ya Rahaleo amewashukuru wanawake hao kwa kumuwezesha baiskeli ambayo itamasaidia kufika shuleni kwa wakati.
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanafanyika kila mwaka ifikapo Machi 8 na katika Mkoa wa Mtwara sherehe hizi zinafanyika Wilayani Masasi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.