Manispaa ya Mtwara- Mikindani tumeendelea kunufaisha Vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa kutoa Mkopo wa shilingi 205,047,000 na vyombo vya usafiri (bajaji na pikipiki) kwa vikundi 52 vyenye jumala ya wanufaika 260.
Mikopo hiyo iliyotolewa Julai 8, 2021 na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya katika viwanja vya Mashujaa imelenga kukuza mitaji ya walengwa hao itakayokusaidia kuwainua kiuchumi.
Akiliwasilisha taarifa ya utoaji wa Mikopo Bi. Juliana Manyama amesema kuwa katika Mkopo ulitolewa unaenda kunufaisha Vikundi 52 vikiwemo Vikundi 39 vya wanawake vilivyopata 27, 825,000 na Vikundi 8 vya walemavu vilivyopata 21,750,000.
Amesema kuwa pamoja na Manispaa kukopesha fedha hizo bado kuna changamoto ya wanavikundi hao kutorejesha mkopo kwa wakati pamoja na jitihada na ufuatiliaji zinazoendelea kufanyika ikiwemo kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaoshindwa kurejesha Mikopo kwa wakati.
Katika mwaka wa fedgha wa 2020/2021 Manispaa ya Mtwara- Mikindani kupitai mfuko wa wanawake , Vijana na Watu wenye Ulemavu tumekopesha 420,647,000 kati ya Milioni 399,836,198 zilizopangwa kwenye bajeti hiyo sawa na asilimia 100
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.