Vikundi 35 vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu vinavyotarajia kupata mkopo wa asilimia kumi kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani vimepatiwa mafunzo ya kuwajenge auwezo juu ya matumizi sahihi ya fedha watakazokopeshwa ili kutimiza malengo waliyokusudia.
Pamoja na matumizi sahihi ya fedha vikundi hvyo pia vimefundishwa ujasiriamali , utunzaji wa fedha , uongozi bora na kuwajengea uwezo ili waweze kuwa wafanyabiashara wenye tija.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Juliana Manyama amesema kuwa Mnaispaa inatoa mafunzo hayo ili kuhakikisha lengo la Serikali lakusidia vikundi linatekelezeka.
Amesema kuwa mafunzo hayo pia yanalenga kuwajulisha wanavikundi fursa zilizopo ili waweze kunufaika nazo ikiwemo kupata mikopo mbalimbali tofauti na inayotolewa na Halmashauri.
Manispaa ya Mtwara-mikindani inatarajia kutoa mkopo wa shilingi milioni mia mnbili arobaini na nne (244,000,000) kwa vikundi 35 vya wajasiriamali vikiwemo vikundin24 vya wanawake, 4 vya vijana na watu wenye ulemavu 7.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.