Katika kuhitimisha Maadhamisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya amegawa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa vituo vya Afya Pamoja na wanawake wazee, na wenye mahitaji maalum ndani ya Manispaa Mtwara Mikindani.
Msaada huo ulitikana na nguvu ya michango ya wadau mbalimbali wa manispaa hiyo ni Pamoja na mashuka, mabati, godoro, jiko la gesi, vifaa vya usafi, mchele, unga, sukari, sabuni za unga na vingine vingi.
Akifafanua kuhusiana na msaada huo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Fatuma Msuya amesema msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kama Idara ilijikita kuhakikisha wanashika mkono jamii yenye uhitaji.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 08 na mwaka huu kauli mbiu yake ni “wanawake na Wasichana: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.