Wàsimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata na Mitaa wametakiwa kuacha Kufanya kazi Kwa mazoea badala yake wanatakiwa kuzingatia matakwa ya Sheria, Kanuni na Miongozo iliyowekwa kwenye zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Rai hiyo imetolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kwenye mafunzo yanayotolewa kwa wàsimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata na Mitaa Leo Novemba 30,2024 katika Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi.
Aidha Mwalimu Nyange amewataka wàsimamizi hao kujitambua na kujiamini katika Utekelezaji wa majukumu yao na kutosita kushirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa Uchaguzi katika masuala ambayo wanastahili kushirikishwa.
Amewataka kutambua dhamana kubwa waliyopewa na Serikali katika Kufanya kazi ya Uchaguzi kwa maslahi ya Taifa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.