Kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Manispaa ya Mtwara-Mikindani wametakiwa kufuata miongozo,taratibu na sheria za uchaguzi zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kufanya uchaguzi huo kuwa huru, wa haki na wenye kuaminika.
Rai hiyo imetolewa August 7,2020 na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mtwara Mjini Col. Emanuel Mwaigobeko wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na wasimamizi hao kilichofanyika katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara.
Mwaigobeko amesema kuwa Timu yake imejipanga vema katika kuhakikisha kuwa kila kitu kitakachofanyika katika uchaguzi kinakuwa wazi hatua kwa hatua ili kupunguza malalamiko yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wake Bwana Benezigwa Rushita Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata amesema kuwa wamejipanga kuyafanyia kazi yale yote watakayoelekezwa na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kuzingatia miongozo na sheria zilizopo ili kutenda haki kwa watu wote.
Nae Hadija Mkongo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Chuno amesema kuwa wamejiandaa kupokea mafunzo hayo na kuahidi kuyasimamia maelekezo yote kuelekea uchaguzi na kuhakikisha kuwa wanatenda haki .
Katika Mafunzo hayo wasimamizi wasaidizi thelathini na sita wamepatiwa mafunzo na kula viapo viwili vikiwemo kiapo cha kujitoa uanachama na kiapo cha kutunza siri ikiwa ni utayari wa wao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizopo.
Mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa Uchagzui yatafanyika kwa siku tatu kuanzia Agosti 7,2020 na yanatarajia kukamilika Agosti 9,2020.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.