Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Thoams Salala akizunumza na makarani watakaofanya kazi kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi
Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Thomas Salala amewataka makarani wa sensa,wasimamizi wa maudhui ya sensa na wataalamu wa TEHAMA ngazi ya Kata kuhakikisha wanakuwa wazalendo wanapoenda kufanya kazi ya uingizaji wa taarifa kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi ili kupata takwimu sahihi zitakazotumika kwenye kupanga mipango ya mendeleo ya Taifa. linalotarajia kufanyika Agosti 23, 2022.
Salala ametoa wito huo leo Agosti 15,2022 kwenye mafunzo elekezi ya makarani wa sensa yanayoendelea kufanyika Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Stella Maris kilichopo Mtwara.
Aidha Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuliendea zoezi hilo kwa umakini mkubwa huku wakitambu kuwa Taifa limewapa dhamana kubwa ya kufanya kazi hiyo ya sensa kwa niaba ya watanzania.
“Kazi mnayoenda kuifanya ni kubwa, ya kiwango kikubwa, yenye maslahi mapana ya nchi yetu leo kesho na kesho kutwa,mkaifanye kwa uangalifu kwa faida ya kwetu sote’amesema Salala.
Aidha amewahakikishia washiriki hao ushirikiano mkubwa na ulinzi wa kutosha kwenye zoezi hilo na amewataka kutoa taarifa mapema kwa mwenyekiti wa sensa wa Wilaya pale watakapokutana na changamoto yoyote.
Akizungumza kwa niaba ya Makarani wenzake Bwana Mohamedi Nguyahambi ameishukuru Serikali kwa kuwachagua kuifanya kazi hiyo kubwa na muhimu kwa Taifa na ameuhakikishia uongozi wa Mkoa na Wilaya kuwa wanaenda kuifanya kazi hiyo kwa uadilifu na kwa kuzingatia yale yote waliyofundishwa.
Mafunzo elekezi ya Uingizaji taarifa kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi Manispaa ya Mtwara-Mikindani yameanza Julai 31 na yatamalazikia Agosti 18, 2022
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.