Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameahidi kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi wote ambao watashindwa kuwapeleka Watoto shule hadi kufikia jumatatu ya tarehe 28 Machi 2022.
Mhe. Kyobya ameyasema hayo Machi 28,2022 alipokuwa kwenye wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika eneo la uwanja wa mbae katika Kata ya Ufukoni iliyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha katika kuhakikisha kuwa Watoto waliopo shuleni wanasoma vizuri amesisitiza kamati za shule kuhakikisha zinahamasisha wazazi kuchangia chakula cha mtoto shuleni na kuiagiza ofisi ya elimu kutoka manispaa kuweka mikakati mizuri ya wazazi hao kuchangia fedha fedha au kupeleka chakula shuleni.
Sambamba na hilo amewataka wananchiwa Kat ahiyo na viongozi wao kutafuta eneo la ujenzi wa shule na kuanza kuchangishana fedha za ujenzi ili serikali iweze kutia mkono na kata iweze kuondokana na changamoto ya uhaba wa shule.
Kuhusu zoezi linaloendelea la anuani za makazi Mhe. Kyobya amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaopita kwenye maeneo yao kukusanya taarifa mbalimbali muhimu.
Ameendelea kuwajulisha uwepo wa sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika Agosti mwaka huu na kuwataka kujiandaa kwa ajili ya kuhesabiwa ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya pia amewataka wananchi hao kuchangamkia fursa pindi Mwenge wa Uhuru utakapowasili ndani ya Manispaa Aprili 24 mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa ziara zake aanzozifanya za kusikiliza kero ya wananchi na amemuahidi kuyafanyika kazi maagizo yote aliyoyatoa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.