Katika kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani, wataalamu wa afya katika kituo cha afya cha Ufukoni kilichopo Manispaa ya Mtwara- Mikindani wametoa elimu kwa Wanawake wanaonyonyesha juu ya umuhimu wa maziwa ya mama pekee kwa Watoto ndani ya miezi sita ya ukuaji wa Watoto.
Akitoa Elimu hiyo leo Agosti 2,2024 Kituoni hapo Muuguzi Mkunga Bi. Salima Hiyara amewataka Wanawake hao wanaonyonyesha kuondokana na mila potofu katika malezi ya ukuaji wa mtoto zikiwemo matibabu ya macho kwa watoto wachanga kupitia maziwa ya mama pamoja na kumkosesha mtoto maziwa ya mwanzo kwa kuyakamua na kuyamwaga.
Elimu hiyo imeambatana na utoaji wa chanjo mbalimbali za kumkinga mtoto mchanga dhidi ya magonjwa mbalibali kama vile BCG, OPV, rotavac, MR, DPT, PVC pamoja na upimaji wa uzito na MUAC kwa ajili ya kubaini hali ya lishe na ukuaji wa mtoto.
Maadhimisho hayo yameanza agosti 1, 2024 ambapo kilele chake kitakuwa Agosti 7,2024 katika viwanja vya Kanisa la EAGT Rahaleo yakiwa na Kauli mbiu inayosema kuwa ‘’Tatua changamoto saidia unyonyeshaji’’
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.