Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa sehemu ya kwanza ya mpango wa TASAF ikiwemo uwepo wa kaya hewa na zisizo na sifa, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Dunstan Kyobya amewataka wawezeshaji wa sehemu ya pili ya mpango huo awamu ya tatu kuhakikisha wanaibua kaya masikini zenye sifa vinginevyo watakaokiuka watachukuliwa hatua.
Kyobya ameyasema hayo April 19, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kawaida alipofanya ufunguzi wa kikao kazi cha kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa sehemu ya pili ya TASAF awamu ya tatu.
Amewataka wawezeshaji hao kuzingatia kanuni na miongozo wanapokwenda kuibua kaya masikini ili kutimiza malengo ya serikali ya kuhakikisha fedha zitakazotolewa zinaenda kuwanufaisha walengwa ikiwemo kupunguza umasikini na kuongeza ukuaji wa uchumi.
Aidha Kyobya amewasisitza wawezeshaji kushirikisha viongozi wote waliopo kwenye Kata Pamoja na wataalamu waliopo halmashauri ili kuondoa uonevu na manung’uniko ya hapa na pale katika utekelezaji wa zoezi hili.
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile ameishukuru Serikali kwa kutuletea tena mradi wa TASAF na kuwasisitiza watendaji wanaoenda kufanya kazi ya kuwatambua walengwa kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa weledi ili kuondoa changamoto zilizowahi kujitokeza katika awamu iliyopita.
Kwa upande wake Bwana Ladislaus Mwamanga Mkurugenzi mtendaji wa TASAF katika hotuba yake amesema kuwa Serikali imeamua kuendelea na kipindi cha pili katika awamu ya tatu ya TASAF ili kuhakikisha kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zinapata usaidizi wa Serikali kupitia mradi huu kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umasikini.
Amesema kuwa Mpango huu wa sasa unaenda kutekelezwa katika halmashauri zote 184 za Tanzania bara na wilaya za zanziba huku utekelezaji wake ukihusisha vijiji na mitaa yote iliyopo nchini Pamoja na maeneo ambayo hayakupata fursa katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wa mradi.
Mwamanga ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha pili cha awamu ya tatu kitafikia kaya zipatazo milioni moja na laki nne na nusu zenye jumla ya watu Zaidi ya milioni saba huku Mnaispaa ya Mtwara Mikindani ikitarajia kuandikisha kaya zipatazo……..
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.