Baada ya wafanyabiashara wanaofanya biashara zao eneo la soko Kuu lililopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kugoma kufungua maduka yao Juni 6,2022 kwa madai ya kupunguziwa pango la vibanda, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wafanyabiashara hao kufungua maduka yao na kuendelea na biashara kama kawaida huku akimuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mtwara kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaohamasisha mgomo kwa wafanyabiashara hao.
Wafanya baishara hao wameiomba Manispaa kuwapunguzia pango la vibanda kutoka shilingi elfu arobaini (40,000) ya mabanda makubwa wanayolipa sasa hadi shilingi elfu ishirini na tano (25,000) na mabanda madogo kutoka shilingi elfu ishirini na tano (25,000 ) hadi shilingi elkfu kumi na tano(15,000)
Aidha Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi kuyafanyia kazi madai hayo huku akimsisitiza kuendelea kukusanya pango la vibanda kwenye eneo hilo ili Manispaa iweze kupata mapato yake na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mhe. Kyobya pia amewataka wafanyabiashara wote ambao wanadaiwa pango la vibanda na Manispaa kulipa kodi hiyo mara moja kama mkataba unavyosema.
Katika eneo la soko Manispaa hadi sasa inadai pango la vibanda kiasi cha shilingi milioni mia moja thelathini na sita laki nne kumi na tano elfu na shilingi mia nane ( 136,415,800)
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.