MD NYANGE AWATAKA WATENDAJI WA KATA NA MITAA KUWASAKA WALIOTELEKEZA VIWANJA
Mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan B.Nyange ametoa agizo kwa watendaji wa Kata na Mitaa wa Kata ya Mtawanya kuhakikisha wanawatafuta walimiki wa viwanja waliotelekeza maeneo yao na kubaki kuwa pori kwa muda mrefu waweze kuyafanyia usafi ili kuondoa kero mbalimbali ikiwemo uwepo wa vibaka na nyoka.
Akizungumza katika Mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya Mtawanya uliofanyika leo Machi 18,2024 katika viwanja vya Mahakama ya mwanzo ya Mtwanya Nyange alisema kuwa Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Mtwara alianzisha jogging kwa ajili ya kuhamasisha usafi kata kwa kata hivyo itakapofika zamu ya mtawanya atapita kukagua hali ya mazingira kwenye nyumba za watu binafsi.
Akitolea ufafanuzi wa kero wanazopata wanawake katika huduma ya uzazi katika Kituo cha afya cha Likombe hususani kero ya kutozwa fedha wakati wa kujifungua na malipo kwa huduma ya matibabu kwa Watoto wenye umri kuanzia 0 hadi miaka mitano,aliwataka wananchi kutoa taarifa kupitia namba ya simu ya mkononi ili aweze kufanyia kazi kwa wakati.
Nyange Amesisitiza jamii kuendelea kuwalinda Watoto wa kike dhidi vijana haribifu (wahuni) ambao kwa makusudi hudhamilia kuzima ndoto za Watoto hao.
Diwani wa Kata ya Mtwanya Mhe. Ahmed Kalikumbe ametoa rai kwa wananchi wa Mtwanya kutimiza wajibu wao kwa kufanya usafi bila shuruti na kusimamia Watoto wao kuzingatia masomo pasipo kusubiri serikali huku akimuomba Mkurugenzi kuongeza walimu katika shule ya msingi ya mtwanya kutokana na upungufu wa walimu uliopo shuleni hapo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.