Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mei 7,2018 imeendesha mafunzoya siku tatu kwa watoa huduma, wenyeviti na wajumbe wa kamati za afya kwa ajili ya kupeana uelewa wa maswala yanayohusu mfuko wa afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uweo watoa huduma hao ili waweze kufahamu mfumo mzima wa CHF iliyoboreshwa pamoja na matumizi ya mfumo huo ambao utakatumika kuandikisha wananchi katika mfumo huo ujulikanao kama Insurance Management Information system(IMIS)
Dkt Christa Nzali kaimu mganga mkuu wa manipsaa amesema kuwa uanzishwaji wa CHF iliyoboreshwa imekuja kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zinajitokeza kwenye mfuko wa afya ya jamii ujulikanao TIKA yaani tiba kwa kadi ambao unatumika hadi sasa.
Amesema mfumo huo utakapoanza kila kaya itachangia shilingi 30,000 kwa mwaka ambayo itahusisha walengwa sita wakiwemo baba, mama, mke, mume pamoja na watoto wenye umri usiozidi miaka 18. Ameongeza kuwa mwananchi anapokata bima hiyo atatibiwa katika Zahanati,Vituo vya afya na hospitali zote za wilaya, mikoa yote iliyopo Tanzania isipokuwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mafunzo ya CHF iliyoboreshwa yameanza mei 7 na yataishia mei 9, 2018 na baada ya hapo mafunzo yataeendelea kwenye ngazi nyingine zilizopo kwenye Kata. Aidha huduma za CHF iliyoboreshwa itaanza kufanya kazi ifikapo mwezi Julai 2018.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.