WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WAPATIWA KADI ZA TIKA.
Watoto 100 waishio katika mazingira hatarishi Manispaa ya Mtwara Mikindani wamepatiwa kadi za bima ya afya (TIKA) zenye thamani ya Tsh.500,000 ili ziweze kuwasaidia kupata matibabu bure pale wanapougua.
Kadi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani na kugawiwa na Mh diwani wa Kata ya majengo Ziha Khalidi, kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Majengo Tarehe 15 Juni 2017.
Akigawa kadi hizo Ziha khalidi alisema kuwa wazazi wanapaswa kuzitunza kadi, kwani zitasaidia watoto kutibiwa bure pale wanapopata homa kama vile malaria n.k. Pia alimshukuru Mkurugenzi kwa kitendo alichokifanya kwani amesaidia kuokoa maisha ya watoto wetu.
Vile vile Diwani huyo aliwataka watoto kutambua haki zao na pale inapotokea wanafanyiwa vitendo vya ukatili waende wakaripoti kwenye Serikali za Mitaa kwani sheria zipo .
“Ninafahamu kuna watoto wengi wanaishi na baba au mama wa kambo majumbani, mnanyanyaswa na wengine mnabakwa hasa watoto wa kike, msiogope kimbilieni Serikali za Mitaa mkatoe tarifa”alisema zikha khalidi.
Awali wakisoma risala kwa niaba ya watoto wenzao ,wanafunzi wanaolelewa kwenye kituo cha yatoto yatima cha EAGT wamekusudia kuufikishia umma wananchi wa mtwara maswala yahusuyo Ulinzi na Usalama wa mtoto. Wamesema kuwa ili mtoto awe salama anahitaji Kujulikana, Kutambulika na kupendwa.
Aidha watoto hao walitoa wito kwa jamii na Serikali, kuhakikisha kuwa mtoto haachwi ana zurura mitaani muda wa masomo, kuzuia watoto kununua vileo na sigara, kuepuka kuongea masuala ya kiutu uzima ikiwemo kutamka matusi mbele ya watoto, Kuacha kupigana na kutoleana lugha za matusi mbele ya watoto, Kuhakikisha watoto wanaangalia vipindi vya maadili mema katika luninga zetu, na kuwzauia watoto kuingia katika kumbi za Starehe na kuangalia filamu zisizo na maadili.
Naye Rose Mlaki Mratibu wa Mfuko wa afya ya Afya Manispaa Mtwara- Mikindani amesema kuwa kadi hizo zitatumika bure kwenye Vituo vya afya na Zahanati za serikali tu zilizopo Manispaa. Na kwamba kadi hizo zitadumu kwa mwaka mmoja tu.
Pia amewahamasisha wazazi na walezi waliokusanyika kwenye viwanja hivyo na ambao hawana kadi za afya, kuhakikisha kuwa wanakata bima za afya kwa za kwao au watoto wao kwa gharama ya Tsh. 5000/= kwa kila mmoja.
Siku ya Mtoto wa Afrika huazimishwa kila mwaka Tarehe 16 Juni ikiwa ni kumbukumbu ya Mauaji ya watoto yaliyofanywa na Utawala wa Makaburu huko Soweto .Afrika ya Kusini Tarehe 16 Juni 1976. Katika tukio hilo inakadiriwa kuwa watoto wapato 2000 waliuawa. Adha Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “MAENDELEO ENDELEVU 2030:IMARISHA ULINZI NA FURSA SAWA KWA WATOTO”. Maazimisho hayo yalitanguliwa na warsha iliyohusisha wadau mbalimbali na kujadili mawsala yanayowahusu watoto pamoja na haki za wanawake, lakini pia Wanafunzi was Shule za Sekondari na Msingi walifuundishwa masuala ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.