Ikiwa leo imefikia siku ya tatu tangu Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa chanjo ya polio kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano ianze Mei 18 Mwaka huu. Manispaaa ya Mtwara-Mtwara Mikindani imechanja Watoto 13489 kati ya Watoto 15760 Waliolengwa sawa na asilimia 85.6
Manispaa ya Mtwara Mikindani tunaendelea kuwasisitiza wazazi na walezi kuwapeleka Watoto walio bado kupata chanjo kwenye vituo vya kutolea Chanjo vilivyoandaliwa lakini pia kuendelea kutoa ushirikiano kwa watoa huduma ambao wanapita nyumba nyumba kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo.
Zoezi la Utoaji wa Chanjo ya Polio linaendelea na linatarajia kukamilika ifikapo Mei 21, 2022
“Mzuie mtoto na ugonjwa wa kupooza kwa kumpatia Chanjo ya Polio”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.