Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko amewataka watumishi wa Manispaa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kila mara wanapotekelza majukumu yao na kuwasiistiza kufanya kazi kwa ushirikiano ili halmashauri yetu iweze kusonga mbele .
Mkurugenzi ametoa wito huo Mei 6,2022 kwenye kikao kazi na cha kukumbashana utendaji wa kazi kilichohusisha watumishi wa idara zote zilizopo Makao makuu ya halmashauri.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa rasilimaliwatu Bi. Upendo Haule amesema kuwa watumishi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanatoa huduma bora bila upendeleo kwa kila mwananchi ili kuondoa malalamiko.
Bi. Upendo amewasisitiza watumishi hao kuipenda kazi waliyonayo kwa kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa na serikali ili kuimarisha utawala bora .
Aidha amewasisitiza watumishi kutoridhika na nafasi walizonazo badala yake wajiendeleze kimasomo pale wanapopata nafasi na kuchukua likizo ya mapumziko iliyowekwa kisheria na Serikali ili mtumishi apate muda wa kupumzika na kufanya majukumu mengine ya kifamilia.
Aidha amewataka watumishi kuwa na utii kwa Serikali iliyopo madarakani na kutochanganya siasa na kazi wawapo kazini huku wakizingatia waraka wa mavazi, utunzaji wa siri pamoja na matumizi sahihi ya taarifa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.