Watumishi wa Manispaa Mtwara-Mikindani wamesema michezo baina ya Watumishi ni muhimu katika kuleta umoja, ushirikiano na mshikamano kazini na kupelekea ufanisi katika kazi.
Wameyasema hayo jana baada ya bonanza la 'Nyerere Day' na hamasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lililoandaliwa na Manispaa Mtwara-Mikindani kushirikisha timu za Watumishi Mashabiki wa Yanga na Simba katika Michezo mbalimbali iliyofanyika Uwanja wa Nangwandwa Sijaona.
Gwakisa Mwasyeba, Mkuu wa idara ya Mipango na Uratibu, Manispaa Mtwara-Mikindani alipongeza uwepo wa Bonanza hilo akisema mbali na kujenga afya lakini imekua vyema kukutana watumishi wa idara mbalimbali na kubadilishana mawazo.
Kwa upande wake, Ally Ayoubu, Mwalimu Shule ya Msingi Shangani alisema imekua fursa nzuri kuendeleza mshikamano na umoja baina ya Watumishi na kupata marafiki wapya.
Naye, Ursula Kayombo, Afisa Michezo Manispaa Mtwara-Mikindani alitoa rai kwa washiriki kuendeleza tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuwa na afya njema itakayopelekea ufanisi katika utendaji wao kazini.
Aidha, alitoa rai kwa michezo hiyo kufanyika kila mwisho wa mwezi ili kujenga utamaduni wa Watumishi kupenda michezo na kuendeleza umoja na mshikamano baina yao.
Bonanza hilo likishirikisha michezo mbalimbali iliwemo mpira wa miguu, netboll, kukimbiza kuku pamoja na kuvuta kamba.
#serikalizamitaasautiyawananchijitokezekushirikiuchaguzi
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.