Watumishi wa afya Kituo cha afya likombe wametakiwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya KItuo hiko pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa fedha kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa taarifa za wagonjwa na vifaa tiba (GoT-HOMIS) ili kituo kiweze kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo upatikanjai wa dawa pamoja na ulipaji wa stahiki za watumishiwa kituo hikoi li kupunguza changamoto na malamiko mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani mwalimu Hassan Nyange alipofanya kikao na watumishi hao leo Machi 1, 2024.
Aidha Mwalimu Nyange amewasihi watoa huduma hao kufanya kazi na kuwahudumia wananchi kw auadilisfu na kwa upendo huku akiwasisitiza kutounjika moyo na hoja mbalimbali zinazotolewa dhidi yao.
“Ninatambua kazi kubwa na nzuri mnayoifanya, thamani yenu ipo, fanyeni kazi kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zinavyoelekeza nitawalinda , pale ambapo nitaona hamjatendewa haki” amesema Mwalimu Nyane.
Aidha amewasiistiza watu w akada zote kuheshimiana bila kuangalia kada walizopo na nafasi walizonazo huku akiawaaidi kuwlaipa madeni yao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.