Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange amewaasa Watumishi wapya wa Halmashauri hiyo kuwa waadilifu na kujiamini katika utendaji wao ili kuendana na kasi itakayoleta mchango chanya katika muda wao wote wa Utumishi.
MD Nyange ameyasema hayo wakati wa Mafunzo ya siku moja kuhusu Mfumo wa Ujifunzaji Kieletroniki (MUKI) kwa Watumishi Wapya yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Akifafanua zaidi alisema Utumishi wa Umma kwao ni fursa muhimu ya kujijenga kiutendaji na kuacha alama katika Utumishi zitakazokumbukwa daima na kuisaidia Halmashauri hiyo kufikia malengo yake.
Ameongeza kuwa wakiwa katika nafasi zao wazingatie usawa katika kutoa huduma bila ubaguzi wa aina yeyote huku akiwaahidi kuwapa ushirikiano watakaouhitaji katika kipindi chote cha utumishi wao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, George Mbogo, akielezea kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo alisema yatakuwa na tija kwa watendaji hao kwani kazi nyingi kwa sasa zinafanyika Kieletroniki.
Alisema mada zitakazofundishwa ni pamoja na Mfumo wa Serikali za Mitaa, Sheria zinazosimamia utumishi wa Umma, Haki na wajibu wa mtumishi wa Umma, Kanuni na Maadili ya Utumishi na nyingingine nyingi.
Jumla ya watumishi wapya 40 wamehudhuria mafunzo hayo ambapo kati yao Watendaji wa Mitaa 30, Madereva watatu, Waandishi Waendesha Ofisi wanne pamoja na Wasaidizi wa kumbukumbu watatu.
#TUNATEKELEZA
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.