Kuelekea kilele cha Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani, Mjumbe Kamati ya Utekelezaji wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mtwara Mjini, Bi. Asha Mbani amewaongoza Viongozi na Wanawake wa Kata ya Likombe kukabidhi vifaa na mahitaji mbalimbali katika wodi ya Wazazi (Matenity ward) katika kituo cha afya Likombe.
Akiongozana na Diwani Viti Maalum wa Kata Rahaleo, Mhe. Bhahia Abubakari na Diwani wa kata hiyo, Mhe. Said Seifu, wamesema Lengo ni kutambua mchango wa Wanawake katika Jamii kwa kuwapatia mahitaji yote stahiki wakati wa kujifungua sambamba na kuwapunguzia gharama baada ya kujifungua.
Wamesema jumla ya wanawake 24 wamepatiwa mahitaji zikiwemo Nepi za kisasa 'Diapers', Sabuni za unga, Sabuni za Kuongea, na Dawa za Meno 'toothpaste'.
Vilevile, wamekabidhi Taulo za kike na kalamu za wino kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Likombe sambamba na kushiriki kufanya usafi wa mazingira katika eneo la kituo cha afya Likombe.
Wamesema msaada huo umetokana na nguvu za michango kutoka kwa viongozi hao pamoja Wanawake wa kata hiyo.
Kaulimbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” ambayo imetokana na Kaulimbiu ya Kimataifa ‘’For All Women and Girls, Equality, Rights, Empowerment’’.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.