Cecilia Mapunda Muuguzi wa kutoka kituo cha afya Likombe akitoa chanjo kwa wanafunzi halima yahya katika uzinduzi wa wiki ya chanjo Kitaifa
Katika kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi na kuokoa uhai wa watoto hapo baadae ,wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma ili wakapate chanjo hizo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa chanjo hizo ziliziofanyika April 23 ,2018 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Umoja, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi Edith Shayo amesema kuwa mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata chanjo hizo kwa wakati.
Amesema kuwa Ugonjwa wa saratani ya kizazi ni ugonjwa wa pili unaoongoza kwa kuua wanawake wengi nchini ukitanguliwa na saratani ya matiti hivyo kila halmashauri ihakikishe inawapatia wasichana hao chanjo ya saratani ya mlango kwa kizazi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi Edith Shayo akimkabidhi chanjo muuguzi kama uzinduzi wa chanjo hiyo
Nae Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani bi Beatrice Dominic Dominic amewaomba wazazi, walezi pamoja na watalamu kuwa mabalozi na kuhamasisha jamii yote juu ya umuhimu wa kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kutolea chanjo ili wakapate chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa kuwa chanjo hiyo ina manufaa kwa jamii yetu.
Aidha amesema kuwa chanjo ya saratani ya kizazi inaweza ikaleta mabadiliko kidogo kwa mtoto aliyechanjwa hivyo amewataka kutoogopa kwani mabadiliko hayo ni ya muda mfupi na hayana madhara yoyote katika mwili wa mwanadamu.
Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani bi Beatrice Dominic akimkabidhi chanjo muuguzi cecil mapunda
Awali akisoma taarifa ya Uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi mganga Mkuu wa Manispaa Dkt Joseph Kisala amesema kuwa Saratani ya shingo ya kizazi inaathari kubwa kwa afya ya wanawake na kwamba inakadiriwa wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani hiyo kila mwaka.
Amezitaja dalili za saratani hizo kuwa ni pamoja na kutokwa damu bila mpangilio, kutokwa damu baada ya kujamiiana, maumivu ya mgongo, miguu au kiuno, kupungua uzito, kupungukiwa hamu ya kula, kutokwa na uchafu wa majimaji uliopauka wa rangi ya kahawia au wenye damu ukeni pamoja na kuvimba miguu
Zoezi la utaoji wa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi linaendeshwa Tanzania nzima na lilizinduliwa rasmi April 10,2018 Jijini Dar Es Salaam na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kwa Manispaa Mtwara-Mikindani chanjo hizi zitatolewa katika vituo 14 vya kutolea huduma pamoja na Shule za Msingi na Sekondari. Aidha chanjo hizo.zinatolewa kwa watoto wenye umri wa miaka 14 na Manispaa imekadiria kuchanja watoto takribani 1,131. Wiki ya chanjo imeanza tarehe 23 April na itaishia tarehe 28 April 2018 na baada ya wiki ya chanjokuisha huduma zitatolewa kwa utaratibu wa kawaida kwenye vituo vya afya na kwenye Kata na MITAA
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.