Wazee wa Kimila ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani leo 19/03/2025 wametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Hospitali ya Wilaya Mjimwema na kuelezea kuridhishwa kwao na ujenzi huo.
Wakiongea wakati wa majumuisho ya ziara yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo, wazee hao walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ya ujenzi wa Hospitali hiyo na kuwapongeza wataalamu wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa, Mwalim Hassan Nyange kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, bw. Mipawa Majebele Pamoja na Mganga Mkuu, Manispaa ya Mtwara – Mikindani, Dkt. Elizabeth Oming`o wameahidi kufanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na wazee hao wakati wa ziara yao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.