Kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Manispaa katika kuhakikisha kuwa inawajali wazee hatimae Baraza la wazee waishio Manispaa ya Mtwara imeona na kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na watendaji wake kwa kuweza kufanikisha masuala muhimu yanayowahusu
Katika risala iliyosoma na Katibu wa baraza la wazee bwana Seif Mtapika kwenye uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika Juni 12,2018 kwenye ukumbi wa Manispaa ilitaja masuala muhimu waliyofanyiwa na Manispaa kuwa ni pamoja na kuwakatia bima za afya ya jamii (CHF) ,uundwaji wa mabaraza ya wazee kwenye kata zote pamoja na kufanyika kwa kikao cha kuchagua viongozi.
Evod Mmanda Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ameliomba baraza la wazee lililoundwa kutoacha kulinda maadili na kulipa kipaumbele suala hilo na kuwataka kuwa mstari wa mbele katika kukemea matendo maovu, kuelekeza matendo mema na kuifanya jamii iweze kuwa na maadili mazuri.
“huko tulikotokea sifa ya kuitwa mzee ni kwamba kiwango cha uungwana, maarifa, kujiheshimu na busara kimeongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo hatuna budi kukemea mmomonyoko wa maadili” alisema Mmanda.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani imewatambua wazee wapatao 5798 kwenye zoezi la uhakiki lililofanyika hivi karibuni, na .katika bajeti ya 2017/2018 Manispaa imetumia shilingi Mil. 5 kwa ajili ya kuwasaidia wazee hao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.