Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Stergomena Lawrence Tax ametembelea miradi miwili ya Maendeleo katika sekta ya afya na Elimu yenye gharama ya shilingi Milioni Mia Saba thelathini na nane Mia sita arobaini na Saba Mia tano (738,647,500) ambapo amezindua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Magomeni (177,547,500) na kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Tandika (560,000,000).
Mhe. Waziri ameridhishwa na uimara wa majengo ya miradi hiyo na kupongeza uongozi wa Mkoa, Wilaya na Mkurugenzi kwa kusimamia vizuri.
Mhe.Waziri amefanya ziara Leo Oktoba 6,2024 akiwa sambamba na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Saidi Nyengedi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Patrick Kenani Sawala, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bi.Bahati Geuzye ,Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Abdallah Mwaipaya pamoja viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na watumishi kutoka Taasisi mbalimbali.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.