Kutokana na kuwepo kwa tabia za baadhi ya viongozi kwenye Kata na mItaa kumaliza kienyeji kesi za ukatili wa kijinsia wananzofanyiwa wananwake na Watoto Mstahiki Meya wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani amewataka viongozi hao kuacha tabaia hiyomara moja badala yak e wawapeleke watuhumiwa kwneye vyombo vinavyohusika.
“Wenyeviti wa Mitaa tuepuke kumaliza kesi za ukatili kindugu, tunaendekeza vitendo amabvyo si vizuri, kama mtu anafanya kosa achukuliwe hatua zinazostahili dawati la ji sia lipo, polisi wapo na Mahakam zipo hao ni wahalaifu kama walivyo wahalifu wengine”
Mtsahiki Meya ameyasema hayo
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vinavyoonesha uwepo wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na Watoto ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mstahiki Meya Bi. Shadida Ndile amesema kuwa Manispaa itachukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaobainika kutenda ukatili huo.
“Manispaa ya Mtwara-Mikindani haitavumilia vitendo vya ukatili, tutachukua hatua kwa mtu yeyote atakaebainika kutenda ukatili awe baba, mama au Watoto kwa Watoto wote watashughulikiwa’
Aidha Mstahiki Meya amewasiistiza wananchi kutoa ushirikiano kwenye vyombo husika pamoja na kutoa taarifa pale wanapoona kuna vitendo vya ukatili vinaendelea kwenye maeneo yao ili kujenga ulinzi na usalama wa Watoto na wanawake
Pamoja na hayo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuunda kamati maalumu itakayokuwa inafanya ufuatiliaji mashuleni kuhusu ulinzi na usalama wa wanafunzi huku akiwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawakagua watoto wao kila mara.
Mstahiki Meya ameyasema hayo Novemba 25 alipofanya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.