Wenyeviti na Wajumbe wapya kamati za Mitaa, wametakiwa kuweka tofauti zao za kisiasa pembeni na kushiriki katika kuhamasisha na kuelimisha umma umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange, leo 29/11/2024 wakati wa zoezi la kuwaapisha Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati za Mitaa lililofanyika katika kituo cha Shule ya Sekondari Mtwara Ufundi.
Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 14 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kinaeleza kuwa Mwenyekiti na Wajumbe ndiye mwakilishi wa wananchi kwenye Mtaa aliyochaguliwa hivyo wajipange kwenda kuwatumikia na kutatua kero za wananchi.
"Naomba muelewe ya kuwa Wenyekiti na Wajumbe sio wajiriwa wa Halmashauri, bali ni 'Mwakilishi wa watu', na hivyo anawajibika kwa watu anaowawakilisha na wakazi wa eneo la Mtaa wake,"
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya Salum Naeda, aliwasisitiza wateule wote kwenda kuwatumia wananchi kwa uwezo na moyo wote bila kujali tofauti za itikadi za vyama vyao.
Jumla ya Wenyeviti wa serikali za mitaa 111, Ujumbe Mchanganyiko 333, na Ujumbe wa kundi la Wanawake 222 wamekula kiapo hicho mbele ya Hakimu Mkazi, Mahakama ya Mwanzo Mikindani, Gasper Malisa, akisaidiawa na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Allen Ndomba.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.