Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa kata Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani, wametakiwa kufanya kazi kwa uzalendo, bidii na kushirikiana na kwa kutanguliza maslahi mapana ya nchi.
Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mhe. Shadida Ndile, wakati akifungua kikao cha pamoja cha CMT, Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji Kata kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara (U) - Mwasandube.
Amesema lengo ni kuhakikisha kuwa kiwango cha upatikanaji wa huduma za jamii katika Manispaa kinaongezeka ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Taifa pamoja na kutekeleza Ilani ya Chama Tawala 2020/25.
Kadhalika, Meya Ndile ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji hao kushirikiana na wananchi kutika kutafuta suluihu ya pamoja ya changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Manispaa, Mwalimu Hassan Nyange alihimiza Wenyeviti na Watendaji kutumia kikao hicho kutoa mawazo chanya na ushauri utalakaoleta chachu ya maendeleo katika Manispaa hiyo.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani ina jumla ya Kata 18 na Mitaa 111.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.