Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Dkt. Elizabeth Oming’o amewasisitiza Wenyeviti wa Serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi kujiunga na huduma ya afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF) ili waweze kupata huduma za afya kwa gharama ndogo na kwa uhakika.
Dkt.Oming'o amesema kuwa bima hiyo inapatikana kwa gharama ya shilingi elfu thelathini(30000) kwa mwaka ambapo inajumuisha familia isiyozidi watu sita.
Aidha ametoa rai kwa wenyeviti hao kuwasilisha majina ya wazee wenye sifa kuanzia miaka sitini (60) ili wapatiwe vitambulisho vitakavyowasaidia kupatiwa huduma ya matibabu bure na kwa wakati.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile amemwagiza Mganga Mkuu huyo kuwasisitiza watumishi wa afya walio chini yake kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu za utumishi wa umma ikiwemo matumizi ya fasaha ya lugha kwa wagonjwa.
Hayo yamesemwa Septemba 18,2024 kwenye kikao na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mtwara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.