Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndugu Tito Cholobi amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Wagawa dawa pamoja na wajumbe wa kamati za afya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa anameza dawa za kinga tiba ya magonjwa ya Mabusha, Matende na minyoo ya tumbo ili kutokomeza vimelea vya ugonjwa huo.
Amesema kuwa wananchi wakihamasika kwa wingi kumeza dawa hizo itasaidia kujilinda wenyewe, kulinda wengine na kuwa na afya ya uhakika na kuepusha kutumia gharama kubwa katika matibabu ya magonjwa hayo.
Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Dkt. Elizabeth Oming’o ametoa rai kwa jamii kuacha kupuuzia magonjwa hayo kwa kuwa yana athari kubwa kwa jamii hususani kiafya, kiuchumi, kisaikolojia na unyanyapaa katika familia huku akiwasisitiza wananchi kuelimishana na kukumbushana juu ya umuhimu wa kumeza kinga tiba hizo.
Kwa upande wake Diwani wa kata yaLikombe Mhe. Saidi Seif ameahidi kuhamasisha wananchi katika kata yake kwa kupita nyumba kwa nyumba kuhakikisha kila mwananchi anameza kinga tiba hizo.
Hayo yamesemwa leo Agosti 20,2024 katika uzinduzi wa ugawaji wa kinga tiba za Mabusha, Matende na Minyoo ya tumbo uliofanyika katika mtaa wa Mtepwezi katika kata ya Likombe.
Zoezi la Utoaji wa Utoaji wa Kinga tiba za mabusha, Matende na Minyoo ya tumbo limezinduliwa Leo Agosti 20,2024 na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara na litakamilika Agosti 27, 2024.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.