Wenyeviti wapya wametakiwa kuwa kiunganishi kwa wananchi wa makundi yote bila kubagua ili waweze kufanya kazi vizuri kwa maslahi ya taifa.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile leo Disemba 16, 2024 katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wenyeviti hao walioshinda kwenye Uchaguzi uliofanyika Novemba 27, 2024.
Aliongeza kuwa ni vema wakakumbuka kwamba wananchi wamewaamini na Serikali ina kanuni na Miongozo hivyo hawana budi kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo na sheria za Halmashauri ikiwemo usimamizi mzuri wa mapato ya mitaa yao.
"Muwashirikishe wananchi katika shughuli za maendeleo, simamieni miradi inayokuja katika mitaa na kuwafahamisha wananchi ili wailinde" alisema.
Aidha, aliwataka wenyeviti hao kuishi tabia za kiuongozi ikiwemo kutumia lugha rafiki pamoja na kuepukana na vitendo vya ulevi kwani wananchi wanajifunza kutoka kwao.
Mhe. Ndile pia aliwataka viongozi hao kuendeleza amani na utulivu uliopo kwani viongozi wa mitaa ndio walinzi wa amani kwenye mitaa husika.
Kwa upande wake mratibu wa uchaguzi ngazi ya Mkoa wa Mtwara Bi. Edith Shayo amewataka wenyeviti hao kuzingatia mafunzo ili wakafanye kazi kwa weledi.
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa - LGTI (Hombolo, Dodoma) wakiongozwa na Dkt Natalia Kalimang'asi yalijikita kwenye mada kadhaa ikiwemo, Vikao na Mikutano, Usimamizi wa Ardhi pamoja na Maadili na Uon
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.