Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Bi. Shadida Ndile, amewataka Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa kushirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ili kuimarisha ulinzi na usimamizi wa miradi hiyo.
“Pamoja na kusimamia shughuli za kimaendeleo katika maeneo yetu , tukaoneshe uhitaji wa wananchi katika miradi inayoendelea kutekelezwa ndani ya Kata na Mitaa yetu,hii inaleta uelewa wa pamoja na inamfanya mwananchi kuilinda na kuithamini miradi hiyo”Amesema Mhe.Ndile
Mhe.Ndile ametoa rai hiyo Julai 22, 2021 katika kikao kazi kilichoshirikisha Mkuu wa Police Wilaya( OCD), Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa pamoja na wakuu wa Idara kilichofanyika katika Chuo cha Ualimu-Kawaida (TTC).
Amesema kuwa ili kuleta maendeleo, mwananchi anatakiwa kupata taarifa sahihi juu ya shughuli za kimaendeleo zinazoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ili kuleta hamasa na kuunga mkono juhudi za Serikali.
Katika kufanikisha hilo Mhe.Ndile ameendelea kuwasisitiza watumishi hao kushirikiana na kuwa wabunifu katika kushughulikia changamoto mbalimbali ndani ya jamii ili kuimarisha mahusiano baina yao na kuepuka migogoro isiyo na tija.
Nae Kaimu Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mtwara Bw. Gilbert Kalanje amewataka watumishi hao kuhuhisha na kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika Kata na Mitaa ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.