Wilaya ya Mtwara imejipanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na mashindano ya michezo mbalimbali, Kongamano na Mdahalo wa kujadili maendeleo endelevu ambayo nchi yetu imefikia kwa kipindi cha miaka 63 ya Uhuru.
Maadhimio hayo yamefanywa na Kamati ya Utendaji ya Sherehe za Uhuru Wilaya ya Mtwara ilipokutana leo tarehe 06 Desemba, 2024, kujadili maelekezo mahsusi juu ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara, na kujadili utaratibu wa usimamizi wa sherehe hizo.
Wilaya ya Mtwara ambayo inahusisha Halmashauri tatu za Nanyamba, Manispaa ya Mtwara-Mikindani pamoja na Halmashauri ya Wilaya Mtwara, imeadhimia kufanya michezo hiyo, kongamano na Mdahalo katika Chuo cha Utumishi wa Umma-Mtwara siku hiyo ya tarehe 09 Desemba kwa kuhusisha Viongozi wa serikali, Wazee maarufu, Wafanyakazi wastaafu na wengineo wengi.
Aidha imeadhimia kufanya vipindi maalumu kwenye vyombo vya habari kuhabarisha umma kuhusu sherehe hizo kwa kutumia kauli mbiu iliyotolewa ambayo ni MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA BARA; "UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU".
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.