Kutokana na uwepo wa changamoto ya wananchi wengi kukosa vyeti vya kuzaliwa ndani ya Wilaya ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Dunstan Kyobya ameanzisha Kampeni mahsusi yenye lengo la kuhakikisha wanafunzi, Watoto pamoja na wananchi wote wa Wilaya hiyo wanapatiwa vyeti vya kuzaliwa
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Kampeni hiyo ya siku tatu inahusisha utoaji wa vyeti vya kuzaliwa pamoja na uhakiki wa majina yaliyokosewa kwenye vyeti vya kuzaliwa.
Aidha Mkuu Amewataka Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kuhakikisha Watoto wote wana vyeti vya kuzaliwa na watendaji wa Kata kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kwenda kukata vyeti vya kuzaliwa
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na RITA kwa kubuni jambo la msingi lenye kuleta maendeleo ndani ya Manispaa yetu na kuwaomba watu wenye shida ya vyeti vya kuzaliwa wajitokeze ili wapate vyeti hivyo.
Bi. Juliana Manyama Kaimu Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani amewaomba watendaji wa Kata na mitaa kutoa ushirikiano ta kutoa taarifa kwa wananchi ili wawze kuchangamkia fursa hiyo
Kmapeni ya utojai wav yeti vya kuzaliwa Mnaispaa yaMtwara-Mikindani inafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 31,hadi Novemba 2,2022 ka [IO1] tika Shule ya Msingi Lilungu kwa gharama ya shilingi elfu kumi kwa kila cheti.
[IO1] c
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.