WATOA HUDUMA WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI WA TAARIFA ZA FEDHA NGAZI YA KITUO.
Watoa huduma kutoka sekta ya Elimu na Afya kutoka Manispaa Mtwara-Mikindani na halmashauri ya Wilaya Mtwara wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa Uhasibu na Utoaji wa Taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma.
Mafunzo hayo yana lenga kuwajengea uwezo watoa huduma hao ili kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi katika Halmashauri.
Akiongea kwenye Ufunguzi wa semina hiyo iliyofanyika Jun 8/2017 katika ukumbi wa Tiffany, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani Sambwe Sijabaje alisema kuwa mfumo huu utasaidia kuhakikisha kwamba kunakuwa na muundo maalumu wa kuhifadhia taarifa za mapato na matumizi, hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji wa vituo hivi.
Aliendelea kwa kusema kuwa mfumo huu ni wa aina mbili(kielektroniki na ujazaji wa vitabu ulioboreshwa). Hivyo basi Kwa vituo ambavyo vina changamoto ya umeme na mtandao wahudumu watatakiwa kujaza takwimu katika vitabu na takwimu hizo zitaingizwa katika mfumo kwa ngazi ya halmashauri na vituo vitapatiwa taarifa.
Pia Sijabaje aliwataka wakufunzi kuhakikisha kuwa wanawaelekeza washiriki wa mafunzi hayo kwa undani kuhusu matumizi ya mfumo wa FFARS ili kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa huduma bora vituoni.
Aidha amewataka washiriki baada ya mafunzo hayo watoe taarifa sahihi za mapato na matumizi ambazo zitawekwa kwenye Tovuti za halmashauri ili kuleta uwazi na uwajibikaji.
Mafunzo haya ya siku mbili ya mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha kwenye ngazi ya kituo kwa watoa huduma, yanasimamiwa na Shirika la Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma(ps3) kwa kushirikiana na Tamisemi, na yamehusisha Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Vituo vya afya pamoja na wahasibu wa vituo hivyo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na Manispaa Mtwara Mikindani..
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.