Yaliyojiri kwenye kikao cha Utambulisho Wa Mkuu Wilaya ya Mtwara ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Timu ya Menejiment ya Halmashauri kilichoketi Mei,2020 katika ukumbi wa Manispaa.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.
-Amewaomba Timu ya Menejiment ya halmashauri kumpa ushirikiano katika kipindi atakachohudumu katika nafasi hiyo.
-Suala la kodi ni suala la kila mtu amewataka watumishi kusimamia mapato ya halmashauri kwa kushirkiana
-Kuhusu wafanya baishara kukwepa kulipa kodi amesisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wafanyabiashara ili waendelee kutumia mashine za EFD.
-Tuelimishe wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19
-Katika janga hili la ugonjwa wa CORONA amewataka wanachi kuondoa hofu na kuendelea kufanya kazi na biashara Pamoja na kuizngatia kuongeza kinga ya mwili kwa kula vyakula vinavyoshauriwa vikiwemo tangawizi, ndimu na matunda ya kutosha.
-Amesisitiza uwekaji wa mji katika hali ya usafi nyakati zote hasa katika maeneo ya Taasisi, biashara na makazi.
-Amesisitiza Upandaji wa miti katika maeneo ya mji hususani Miti ya matunda na Vivuli
-Amewataka wananchi kuendelea kushiriki kwenye shughuli za kilimo, Uvuvi na ufugaji ili kujiongezea kipato.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.