SERIKALI YAPANGA KUJENGA MADARASA 12000 KUPITIA MRADI WA BOOST
Ili kuinua na kuboresha ujifunzaji na ufundishaji wa elimu ya awali na Msingi, Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu inatarajia kutumia kujenga madarasa elfu kumi na mbili (12000) pamoja na matundu ya vyoo kwenye shule za awali na Msingi zilizopo Tanzania bara kupitia mradi wa BOOST unaotekelezwa hapa nchini kwa miaka mitano kuanzia 2021/2022 .
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa BOOST Bwana Reuben Swila amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwenye halmashauri zote 184 za Tanzania bara na Mikoa 26 huku Serikali ikitarajia kutumia zaidi ya bilioni 230 kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo katika shule 17,182 za Msingi zilizopo.
Swila ameyasema hayo Desemba 22, 2022 kwenye mafunzo ya kujenga uelewa juu ya mradi wa BOOST yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Kawaida uliopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani yakishirikisha wakishiriki zaidi ya 210 kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akizungumza kwenye Mafunzo hayo Mwalimu Kiduma Mageni Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara ambae pia ni mgeni rasmi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi katika sekta ya elimu ikiwemo shilingi trilioni 1.15 za utekelezaji wa mradi wa BOOST.
Ili mradi huu wa BOOST uweze kutoa matokeo yaliyokusudiwa Mwalimu Mageni amewasihi washiriki wa mafunzo kuumiliki mradi huo ikiwemo kutumia mapato ya ndani ya halmashauri kwenye utekelezaji wake pamoja na kuvisikiliza vizuri vigezo vya mradi na kuvisismamia ili zipatikane fedha za kutosha za utekelezaji wa mradi huo.
Aidha amewasiistiza washiriki kusapoti juhudi za serikali yetu ambayo imewekeza fedha nyingi kwenye elimu kwa hiyo kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya ni kuhakikisha wanasimamaia mradi huo ili matokeo yaonekane.
Mradi wa BOOST unahusisha afua nne ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya awali na Msingi, uimarishaji wa miundombinu ya TEHAMA, mpango wa shule salama kwa shule za Msingi Pamoja na afua zingine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.