Kamati ya Kuthibiti UKIMWI ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani leo tarehe 12 Mei, 2025 imefanya ziara katika vituo vitatu vya Afya kuangalia namna ambavyo vituo hivyo vinatekeleza afua za kudhibiti UKIMWI ngazi ya Jamii ndani ya Manispaa na nchi kwa ujumla.
Ikiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa, Mhemiwa Sixmund Lungu, kamati hiyo imevipongeza vituo hivyo kwa namna vinavyotekeleza majukumu yake katika kudhibiti na UKIMWI sambamba na utoaji wa huduma za kiafya.
Aidha imewataka wahudumu wa afya katika vituo hivyo kuendelea kuelimisha jamii juu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ili kupunguza idadi ya mpya ya waathirika wa ugonjwa huo lakini pia kuendelea kuwaunganisha wenye maambukizi katika kliniki za huduma na tiba matunzo (CTC).
Vituo vya Afya vilivyotembelewa ni leo pamoja na Kituo cha Afya Likombe, Ufukoni na Mikindani.
@mtwarars_habari @ortamisemi @wizara_afyatz @abuu_m_abdullah @sixmund_lungu @maelezonews @zanzibar_aids_commission @tacai
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.