Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL.Patrick Sawala amewataka wanafunzi wanaosoma kidato cha nne katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuzingatia nidhamu kwa walimu na kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu vizuri katika masomo yao, kutengeneza kesho iliyo bora katika Maisha yao na kuweka historia ndani ya Mkoa na Tanzania.
Amesema kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya elimu hapa nchini na kuwataka wanafunzi kuitumia miundombinu hiyo vizuri kwa kujikita kwenye kusoma kwa bidii.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo Leo Januari 27,2025 kwenye kongamano la Elimu kwa wanafunzi wanaosoma kidato cha nne lililofanyika Katika Viwanja vya Mashujaa.
Aidha amewaasa wanafunzi wasichana kutojihusisha na masuala ya ndoa na kuwataka wanafunzi wote kutokuwa watoro na kutokubali kukatishwa tamaa na jambo lolote lile badala yake wawashirikishe walimu wao wa malezi wanapokuatana na changamoto ili wasaidiwe kwenye kuzitatua.
Aidha amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa Mwalimu Hassan Nyange na timu yake kwa kufanya vizuri wakati wote kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya sekta elimu na usimamizi wa miradi na kumtaka kutokata tamaa anapokutana na changamoto zozote badala yake yake ajikite kwenye kuchapa kazi kwa bidii.
Ameendelea kutoa pongezi kwa walimu wote kwa kuwasimamia wanafunzi na kuwafundisha kwa bidiii kulikopelekea Manispaa kufanya vizuri kwenye mitihani yake na amewasisitiza kutokata tamaa kwenye Jambo lolote.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.