Wakati zoezi la utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi na postikodi (opereshieni ya anuni za makazi) likiendelea hapa nchini, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.Jen.Marco Gaguti amewataka watendaji Pamoja na viongozi wa kisiasa wakiwemo madiwani na wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha wanalifanya zoezi hilo kwa muda muda mfupi na kwa ubora unaotakiwa.
Mkuu wa Mkoa ameroa rai hiyo Februari 16,2022 kwenye semina fupi ya kujenga uelewa juu ya mfumo huo iliyofanyika Katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Kawaida.
Akiunga mkono Rai iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ya kufanya kazi kwa muda mfupi, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ametoa siku saba kwa halmashauri tatu za Wilaya ya Mtwara kuhakikisha zoezi la utambuzi wa Mitaa, barabara na uwekaji wa namba kwenye nyumba liwe limekamilika.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi hao (Wenyeviti wa Mitaa, Madiwani na Maafisa watendaji) kufanya mikutanoya uhamasishaji kwenye maeneo yao Pamoja na kuwashirikisha wananchi Katika kufanya utambuzi wa majina ya mitaa, barabara ili kuondokana na malalamiko yasiyo na ulazima.
“Kama kuna maeneo barabara hazina majina mkazipe majina, tunachohitaji mtaa ujulikane na kila nyumba iwe na namba” amesisitiza Kyobya.
Semina fupi ya kujenga uelewa juu ya mfumo wa anuani za makazi inahusisha watumishi na viongozi kutoka halmashauri tatu wakiwemo Kamati ya Ulinzi na usalama, Madiwani , Wakuu wa Idara na Vitengo, Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata, Mitaa , Vijiji na Vitongoji kutoka Wilaya ya Mtwara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.