Mkuu wa Idara ya Mipango na Takwimu Mnaispaa ya Mtwara-MIkindani bwana. Jeremiah Lubeleje akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015-2020 .
Hatimae baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani limefikia ukomo wake na kuvunjwa rasmi Juni 5,2020 baada ya kuhudumu kwa miaka mitano tangu lilipoingia madarakani Oktoba,2015 na kufanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka Bilioni 3.2 mwaka 2015/2016 hadi bilioni 4.9 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 53.7.
Taarifa iliyosomwa na MKuu wa Idara ya Mipango na takwimu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani akimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa bwana Jeremiah Lubeleje katika kikao maalumu cha baraza la Madiwani kilichofanyika Juni 5,2020 , katika Ukumbi wa mikutano wa Call and Vision imesema kuwa, kuongezeka kwa mapato kumetokana na usimamizi mzuri wa baraza la madiwani katika matumizi ya mfumo ukusanyaji wa mapato wa Serikali za Mitaa(LGRCIS) Pamoja na matumizi ya mashine za kukusanyia mapato (POS).
Lubeleje amesema kuwa Pamoja na kuongezeka kwa mapato ya ndani , makusanyo halisi nayo yameendelea kuongezeka kutoka shilingi Bilioni 2.6 mwaka 2015/2016 hadi shilingi Bilioni 4.2 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 57.3
Wakati huo huo bajeti ya Serikali kwa Manispaa ya Mtwara-MIkindani imeongezeka kutoka shilingi Bilioni 23.7 mwaka 2015/2016 hadi Bilioni 33.4 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 41 na kwa upande wa mapokezi ya fedha za Miradi ya Maendeleo, Mishahara na Matumizi mengineyo yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutoka shilingi bilioni 19.3 mwaka 2015/2016 hadi bilioni 28.1 mwaka 2019/2020 sawa na asilimia 46.
Aidha katika usimamizi wa rasilimali fedha Lubeleje amesema kuwa Manispaa imeendelea kufanya vizuri katika usimamizi wa matumizi ya fedha na ufungaji wa hesabu kulikopelekea kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo kutoka mwaka 2015/2016 hadi 2019/2020.
Akielezea kuhusu mikakati iliyowekwa na Manispaa katika ukusanyaji wa mapato amesema kuwa Manispaa imewekeza kwenye miradi Mkakati itakayotumika kama vyanzo vya mapato kama vile ujenzi wa stendi ya mabasi ya Chipuputa,Ukumbi wa kisasa wa mikutano, ujenzi wa eneo la maegesho ya magari Pamoja n akubuni vyanzo vipya vya mapato.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.