Ikiwa kwenye ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mjini imeridhishwa na utekelezaji mzuri wa miradi ya Maendeleo na Ilani.
Akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya ziara hiyo iliyofanyika februari 7, 2020 katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Salumu Mpilu ameipongeza timu ya Menejiment kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi.
“Ninawapongeza Miradi ya leo ni mizuri asilimia 87 hata kama hujaenda shule ukiangalia tu kwa macho unaona kabisa kuwa kazi imefanyika” alisema Mpilu
Aidha Mpilu amewataka watumishi kuendeleza upendo baina yao ili kurahisisha utendaji wa kazi katika Taasisi wanayoitumika ili Ilani iweze kutekelezeka kwa urahisi.
Wakati huo huo Mwenyekiti ameipongeza Shule ya Sekondari ya Sino kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne yam waka kwa kutoa mwnaanfunzi aliyepata daraja la kwanza kwa point nane
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na miradi ya ujenzi wa sehemu ya kupumzikia ya Mashujaa, Stendi ya Mikindani, Ujenzi wa choo cha Milumba, Ujenzi wa madarasa manane Shule ya Msingi kwale, Ujenzi wa Madarasa mawili Shule ya Sekondari ya Sino,Mradi wa maji wa Hiakata pamoja na Lwelu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.