Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko kuvichukulia hatua vikundi nufaika na mkopo wa asilimia kumi wa wanawake ,Vijana na walemavu ambavyo bado havijaresha mikopo licha ya kuongezewa muda wa marejesho.
“Wale ambao bado hawajarejesha mikopo na ambao wamekula fedha za vikundi naomba wabainishwe katika kila kata nakuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, hizi fedha zingeweza kusaidia vikundi vingine ambavyo vinahitaji mikopo.
“Hatuangalii ni mtu wa aina gani, Mkuu wa Wilaya anaedaiwa alipe, Mkurugenzi alipe, hatuangalii tunaangalia makubaliano yetu tuliojiwekea” alisema Kyobya
Ametoa agizo hilo katika kikoa chake na vikundi hivyo kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondariya Call and Vision leo tarehe 4 Juni 2021.
Ameendelea kuwasisitiza wana vikundi hao kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ndani ya muda uliowekwa ili vikundi vingine viweze kunufaika na mikopo hiyo.
Aidha Kyobya amemtaka Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Juliana Manyama kufanya uhakiki yakinifu upya kwa vikundi 191 ambavyo vimenufaika na mkopo huo kwa kukagua hali halisi ya malipo yao, lakini pia kuhakikisha anavitembelea kwenye maeneo yao husika.
Kyobya amewataka watendaji wa Kata zote kuhakikisha wanafuatilia vikundi ambavyo vimerejesha Mikopo na kuwasilisha risiti kwa Mkurugenzi ifikapo Juni 10 mwaka huu.
Aidha ametoa wito kwa vikundi vyote ambavyo tayari vimerejesha mikopo yao lakini bado hawajawasilisha risiti za malipo Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha wanawasilisha risiti zao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.