Ikiwa imebaki takribani miezi miwili nchi ya Tanzania ifanye Uchagzui Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewatoa wasiwasi Wananchi wa Mtwara na kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura kuchagua kiongozi wanayemtaka huku akiwahakikishia uwepo wa amani ya kutosha katika uchaguzi huo.
“Nchi yetu inaingia kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, siku ikifika nendeni mkapige kura ,Ninawahakikishia usalama kwa asilimia 100”alisema Kyobya
Kyobya amesema hayo Agosti 14, 2020 alipofanyaMkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika Kata tano za Tarafa ya Mikindani iliyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha ameahidi kupambana na wale wote ambao wataonekana wana nia ya kuvuruga Uchaguzi kwa kuleta chokochoko na kutishia amani ya watu wengine.
Katika Kuhakikisha yote hayo yanatekelezeka amewaagiza Watendaji wa Kata zote kuhakikisha wanatoa taarifa mapema katika Ofisi yake inapoonekana Kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao ya utawala.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajia kufanyika ifikapo OKtoba 28 mwaka huu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.