Katika kuhakikisha kuwa ufaulu unaongezeka kwa kiwango cha juu kwa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wa kitaifa wa kumaliza kidato cha sita utakaoanza Juni 29 hadi Julai 13 mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameahidi kutoa zawadi ya shilingi Milioni moja kwa kila mwanafunzi atakayefaulu kwa kupata daraja la kwanza pointi tatu kwa shule za Serikali zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Pamoja na zawadi kwa wanafunzi kyobya pia amehidi kutoa shilingi 500,000 kama zawadi kwa mwalimu atakayefaulisha kwa daraja la A katika kila somo ikiwa ni sehemu ya kuwapa motisha na kuwatia moyo kwa kazi kubwa wanazozifanya.
Kyobya ametoa ahadi hizo Juni 15,2020 alipotembelea shule ya sekondari ya wasichana Mtwara na Shule ya Sekondari ya ufundi kwa lengo la kuwapa hamasa wanafunzi, kuwatia moyo na kuwajenga kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani ina wanafunzi 707 waliosajiliwa kwa ajili ya kufanya Mtihani wa kumaliza kidato cha sita kutoka Shule za Sekondari za Mtwara wasichana na Mtwara Ufundi (Shule za Serikali) pamoja na Shule za Sekondari za Aquinas, Amanah na Ocean (Shule za watu binafsi).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.